Friday, 7 June 2019

FANIKIWA KATIKA MAISHA KIJANA.

JINSI GANI KIJANA ANAWEZA KUFANIKIWA KIMAISHA.
 Njia ambazo zinaweza kukusaidia kupata mafanikio kama kijana
MUDA,
-Ili tuweze kufanikiwa katika maisha yetu kama vjana ni vyema kutunza na kutumia mda wetu vizuri, kwa sababu wakati ni Zawadi  kutoka kwa Mungu
-katika maisha yetu ya kila siku muda ni kitu cha muhimu sana kwa sababu unauwezo wa kuuza, kununua chochote katika ulimwengu huu ila sio muda.
-Mambo yanayoweza kusababisha mtu asiutumie mda wake vzuri
ü Kutokuwa na malengo katika maisha yako
-Hii inasababisha mtu asitumi mda wake vizuri kwasababu hanavipaumbele ktk maisha yake.yaani anaishi ili mradi maisha yaende na siku zisogee.
ü Kuairisha mambo
-Unaweza ukamkuta mtu amepanga mambo yake lakini anayahairisha hivyo anajikuta anautumia mda wake vibaya.
ü Kukosa utulivu na maamuzi ya kufanya kitu kimoja baada ya kingine
-Hii nayo inasababisha mtu asitumie mda wake vizuri ktk maisha yake ya kila siku.

WAKATI SAHIHI,
-Pia ili mtu aweze kufanikiwa lazima ajue anaishi ktk nyakati zipi na ni mambo gani ambayo yanampasa kuyafanya, ili tuweze kufikia malengo yetu kama vijana na lazima tufanye mambo kwa wakati sahihi, kwa mfano kama ni wakati wa kusoma, soma na kama ni wakati wa kufanya kazi fanya tena kwa bidii.

JITAMBUE,
- kufanikiwa katika maisha yako ni lazima ujitambue wewe ni nani na unataka nini katika maisha yako, vijana wengi wanapotea na kuanza kulalamika kwasababu hawajajitambua, ukishajitambua ni kwanini mimi ninaishi mpaka sasa hivi wakati kunavijana wa rika langu ambao wamekufa na wengine ni wagonjwa,utajua linalokupasa kufanya ktk maisha yako.
MALENGO,
Njia mojawapo ya kufanikiwa ni kujiwekea malengo ktk maisha yako kwasababu pasipo malengo maisha ya mtu hayana muelekeo, hivyo ni vyema kujiwekea malengo na kuhakikkisha unayafikia na usipo yafikia ujiwekee mikakati ya kuweza kuyafikia mda unaofuata .
JIDHAMINI,
 kufanikiwa ni kupenda kijidhamini,ni vyema kila siku ukatafakari  upowapi katika maisha, unataka kufanya nini katika maisha yako, nini unanachoona uwezi katika maisha yako ili utilie nguvu nyingi uweze kufanikiwa katika hilo unalolouna aliwezekani. kikubwa zaidi usikate tamaa kuwa jasiri kama simba jiamini, jitambue, jikubali kuwa wewe ni wewe unaweza.
MARAFIKI WAZURI, 
Njia mojawapo ya kuweza kufanikiwa ni kuwa na marafiki ambao watakuwa sambamba na wewe kufikia malengo yako kwasababu marafiki wanauwezo mkubwa kudidimiza fikra yako, kwa hiyo kuwa makini sana pale unapochagua marafiki ili uweze tu.

  • USIKATE TAMAA KIJANA JIAMINI UNAWEZA.

No comments:

Post a Comment